Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yaliandikia baraza la usalama ikitaka kesi dhidi ya wakenya sita huko ICC zihairishwe kwa mwaka mmoja

Kenya yaliandikia baraza la usalama ikitaka kesi dhidi ya wakenya sita huko ICC zihairishwe kwa mwaka mmoja

Serikali ya Kenya imelitaka baraza la usalama kujadili barua yake ya hoja ya kutaka kesi dhidi ya raia wake inayoendehswa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ihairishwe.

Akizungumza na mkuu wa Idhaa ya Radio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha, balozi wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Macharia Kamau amesema wanachotaka sio kwamba kesi zifutwe zinazowakabilia maafisa sita wa zamani wa serikali ambao ni Uhuru Kenyatta naibu waziri mkuu, Henry Kosgei, Mohammed Hussein Ali aliyekuwa mkuu wa polisi, William Ruto, Francis Muthaura, na mwandishi habari Joshua Arap sang  bali ziahirishwe kwa mwaka mmoja hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

Amesema zikiendelea sasa zinaweza kuleta chuki na mgawanyiko mkubwa wakati kampeni za uchaguzi mkuu ujao zimeshaanza pia amesema ikiwezekana itakuwa vyema kesi hizo zikaendeshwa nchini Kenya. Na jioni ya leo baraza la usalama limekutana kupitia barua hiyo ya ombi la Kenya. Msikilize balozi Kamau akizungumza na Flora Nducha.