Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchakato wa amani Sudan Kusini ukiendelea, ukiukwaji wa haki waripotiwa

Mchakato wa amani Sudan Kusini ukiendelea, ukiukwaji wa haki waripotiwa

Nchini Sudan Kusini kumeripotiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na pande zote kwenye mzozo ulioanza nchini humo Disemba mwaka 2013. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo, vitendo kama mauaji kinyume cha sheria, ukatili wa kingono, utumikishaji na mashambulizi dhidi ya raia vimeshamiri.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa  pamoja na ofisi ya  haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS imeonyesha kuwa ni maeneo machache sana yenye mzozo ambayo ni salama kama anavyoeleza Ariane Quentier msemaji wa UNMISS.

(Sauti ya Ariane)