Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa Baraza la Usalama wawasili Burundi

Ujumbe wa Baraza la Usalama wawasili Burundi

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa umewasili hii leo jioni nchini Burundi katika juhudi za kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo. Wajumbe hao wanatarajia kukutana hapo kesho kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza

kutoka Bujumbura, Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA anaarifu zaidi.

(Taarifa ya Kibuga)

Ujumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mewasilii hapa Bujumbura saa 11.20 majira na hapa na umeundwa na watu 33 wakiwemo mabalozi 15 wa baraza hilo na wasaidizi wao. Lakini pia Mjumbe mpya wa Umoja wa mataifa Burundi Jamal Ben Omar. Ujumbe huo umepokelewa katika uwanja wa ndege na Waziri wa mambo ya nje Alain Nyamitwe.

Kwenye ratiba , ujumbe huo utakuwa na mazungumzo na wadau mbalimbali wa siasa za Burundi, kuanzia wakuu serikalini , vyama vya kisiasa ikiwa ni pamoja na wapinzani lakini pia mashirika ya kiraia.

Watakuwa pia na mazungumzo hapo kesho ijumaa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika mkoa wa kati wa Karusi halafu kuzungumza na waandishi wa habari siku hiyo hiyo ya ijumaa muda mfupi kabla ya kuondoka.

Kwa mujibu wa duru za umoja wa mataifa, Ujumbe huo utakuwa na shughuli ya kuishawishi serikali ya Burundi ikubali kutumwa nchini humo vikosi vya walinda amani wa Muungano wa Afrika na kufufua mazungumzo yaliokwama kati ya serikali na Upinzani.