Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapongeza chaguzi Afrika Magharibi, likihofia pia usalama

Baraza la usalama lapongeza chaguzi Afrika Magharibi, likihofia pia usalama

Baraza la usalama limekaribisha chaguzi za karibuni zilizofanyika nchini  Nigeria, Togo, Burkina Faso, Guinea na Côte-d'Ivoire, huku pia likisistiza haja ya chaguzi zijazo nchini Niger, Benin, Cabo Verde, Ghana na Gambia kuwa huru, za haki, amani, jumuishi na za kuaminika.

Wajumbe wote 15 wa baraza pia wameelezea hofu yao kwamba mivutano ya kisiasa nchini Guinea-Bissau inaweza kuendelea kumomonyoa serikali nchini humo kuweka hatarini mafanikio yaliyofikiwa na taifa hilo tangu uchaguzi wa 2014.

Katika masuala ya usalama baraza limerejelea kulaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya karibuni hususani Mali na eneo la Sahel, vilevile ziwa Chad ambako mengi yamefanywa na kundi la Boko Haram.