Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kuendesha tafiti kuhusu maambukizi ya Ebola kupitia mbegu za kiume

WHO kuendesha tafiti kuhusu maambukizi ya Ebola kupitia mbegu za kiume

Shirika la afya duniani, WHO kanda ya Afrika limesema tafiti zaidi zinahitajika kufahani ni jinsi gani wanaume waliopona Ebola wanasababisha maambukizi ya kirusi cha homa hiyo hatari kupitia mbegu zao za kiume.

Mkurugenzi wa magonjwa ya kuambukiza wa WHO katika kanda hiyo Magda Robalo amesema hayo akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia wanasayansi wamebaini kirusi hicho kwa baadhi ya wanaume waliopona Ebola.

WHO inataka wanaume waliopona kuendelea kutumia kinga wakati wa kujamiiana hadi awamu mbili za vipimo vya majimaji hayo zitakapathibitisha hakuna kabisa kirusi cha Ebola.

Kwa mantiki hiyo Dokta Magda anasema licha ya Ebola kutangazwa kutokomezwa huko Afrika Magharibi....

Tunapaswa kuendelea kufuatilia hali ilivyo na mwelekeo wake ili kupata uelewa halisi na kuona ni jinsi gani ni jinsi gani maambukizi yanafanyika kutoka kwa wanaume waliopona Ebola na bila shaka hii ni changamoto kubwa kwa nchi husika, WHO na wadau wake. Ni lazima tuendelee kuwa macho.”