Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio dhidi ya AMISOM Somalia

Ban alaani shambulio dhidi ya AMISOM Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi lililotekelezwa asubuhi ya leo katika kituo cha ujumbe wa Afrika nchini Somalia AMISOM mjini El Adde, mkoani Geddo nchini humo.

Idadi ya waathirwa katika shambulio hilo bado inahakikishwa.

Taarifa ya Katibu Mkuu iliyotolewa na ofisi ya msemaji wake inasema kuwa Ban amepongeza juhudi za AMISOM katika kusaka amani Somalia. Huku pia akisema shambulio hilo linalodaiwa kutekelezwa na kundi la Al Shabaab halitatowesha nia ya Umoja wa Mataifa kufanya kazi na AMISOM ili kusaidia Somalia na watu wake.

Awali akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu Stéphane Dujarric amesema walikuwa hawajapokea taarifa kamili na akaongeza.

(SAUTI DUJARRIC)

"Tunafauatili hali na kwa vyovyote vile tunalaani shambulio. Naelewa kuwa wengi wa walioathiriwa ni wanajeshi kutoka Kenya. Tunatuma salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Kenya na kwa wote ambao wameuliwa kwnye shambulio."