Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

PASADA yaleta nuru kwa mtoto Halima anayeishi na VVU

PASADA yaleta nuru kwa mtoto Halima anayeishi na VVU

Harakati za kupambana na Ukimwi zinashika kasi duniani kila uchao. Miongoni mwa harakati hizo ni kuhakikisha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wanapatiwa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo. Mathalani hadi Juni 2015 idadi ya wanaopatiwa dawa hizo walikuwa zaidi ya Milioni 15 na laki Nane ikiwa ni nyongeza kutoka Milioni 13 na Nusu mwaka uliotangulia. Hata hivyo watu wanaoishi na VVU wakiwemo pia watoto wanahitaji msaada zaidi ya dawa pekee. Je ni upi? Na unasaidia nini? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii inayomuangazia mtoto Halima ambaye alizaliwa na VVU lakini hakufahamu hadi alipotimiza umri wa miaka 10.