Walinda amani wa UNAMID waviziwa, wapokonywa silaha

Walinda amani wa UNAMID waviziwa, wapokonywa silaha

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID, umesema kuwa msafara wake wa walinda amani umeviziwa leo na kikundi chenye silaha kisichojulikana, ambapo mlinda amani mmoja amejeruhiwa na silaha kupokonywa.

Tukio hilo limetokea karibu na eneo la Anka, Darfur Kaskazini, mwendo wa takriban kilomita 55 kaskazini mwa mji wa Kutum.

Washambuliaji hao ambao walikuwa wengi zaidi kuliko walinda amani wa UNAMID, pia wameteka mashingani moja, pamoja na bunduki kadhaa na raundi za risasi.

UNAMID imelaani mashambulizi kama hayo dhidi ya walinda amani wake, ikisema inashirikiana na mamlaka za Sudan katika kuchunguza tukio hilo.