Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Urusi na India wametangaza ushirika kufikia malengo ya nishati mbadala:UNEP

Urusi na India wametangaza ushirika kufikia malengo ya nishati mbadala:UNEP

Kampuni ya uzalishaji wa nishati ya jua yaani sola ya India (SECI) na ile ya Urusi (REA) wametia saini makubaliano ya kuanzisha mradi mkubwa wa nishati ya jua nchini India kuanzia mwaka huu wa 2016 hadi mwaka 2022.

Mradi wa majaribio wa megawati 500 utaanza kwanza kama sehemu ya makubaliano. Makampuni hayo mawili yameafikiana njia za utekelezaji wa uzalishaji wa nishati hiyo ya jua na vifaa nchini India. Kampuni ya Urusi REA itachangua teknolojia na ufadhili wa fedha wa gharama ndogo , huku kampuni ya India ya SECI ikijikita katika kuhakikisha inapata kibali na ridhaa kwa ajili na maendeleo ya miradi.

Mpango umeundwa ili kupigia upatu mpango wa serikali ya India ulioanzishwa mwaka 2015 wa kuifanya nchi hiyo kama miongoni mwa mataifa wazalishaji wa duniani ujulikanao kama “Make in India”