Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Filippo Grandi aeleza dira yake kwa UNHCR

Filippo Grandi aeleza dira yake kwa UNHCR

Kamishna Mkuu Mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Filippo Grandi amezungumza leo kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi akieleza mipango anayotaka kutekeleza katika muda wake ili kukabiliana na swala la wakimbizi linalozidi kuongezeka huku idadi yao ikiwa imefika milioni 60.

Mathalani amesisitiza umuhimu wa kutekeleza jukumu la msingi la UNHCR ambalo ni :

(Sauti ya Bwana Grandi)

“ Ni ahadi ya UNHCR ya kuendelea kuwa mtunzaji wa ulinzi wa wakimbizi, ikimaansiha kuhakikisha kwamba wakimbizi wanapata hifadhi wakiwa wameiomba kwa njia halali, na pia wanapoishi ukimbizini, tukitumaini iwe kwa muda mfupi, kuhakikisha kwamba wanaishi maisha yenye usalama na utu.”

Aidha ametaja kuimarisha mifumo ya UNHCR ya kukabiliana na mizozo ya dharura, akisema pia kwamba anataka wakimbizi wawezeshwe kurejea makwao kwa hiari au kusafiri ili kupatiwa pia hifadhi kwenye nchi zingine.

Hatimaye amesema kongamano la kimataifa kuhusu wakimbizi wa Syria litafanyika New York, Marekani mwezi huu ambapo anatumai nchi zingine zitaahidi nafasi zaidi za hifadhi kwa wakimbizi.