Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DR Congo yaorodhesha wakimbizi 6,000 toka Sudan Kusini:

DR Congo yaorodhesha wakimbizi 6,000 toka Sudan Kusini:

Takribani wakimbizi 6,000 wamewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakitokea majimbo ya Equatoria Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR watu hao ambao pia wanajumuisha raia wa Congo wanaongia kwenye eneo la Dungu na walianza kukimbia mwezi Disemba .Nini kilichowachagiza kufungasha virago vyao , Teresa Orango ni afisa habari wa Kanda ya Afrika ya Mashariki na Kati wa UNHCR

(SAUTI YA TERESA ORANGO)

Ameongeza kwamba mbali ya DR Congo sasa wameanza kuingia Afrika ya Mashariki pia

(SAUTI YA TERESA ORANGO 2)