Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka iwezeshwe kufika haraka Taiz ili kutoa misaada ya dharura

WHO yataka iwezeshwe kufika haraka Taiz ili kutoa misaada ya dharura

Shirika la afya duniani, WHO limeelezea wasiwasi juu ya kuzidi kuzorota kwa hali ya kiafya kwenye mji wa Taiz nchini Yemen ambako zaidi ya watu 250,000 wanaishi huku wamezingirwa na vikundi vinavyopigana  tangu mwezi Novemba mwaka jana. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Katika taarifa yake WHO imesema hali si shwari kwani hospitali zote Sita za mji huo zimelazimika kusitisha baadhi ya huduma na nyingine zimezidiwa na idadi kubwa ya wagonjwa.

Halikadhalika kutokana na ukosefu wa usalama, mashirika ya kutoa misaada yanahaha kuwasilisha vitaa tiba na vile vya kufanyia upasuaji.

Mathalani imetolea mfano malori yake Sita yaliyobeba shehena za dawa na vifaa tiba yamezuiwa kuingia mji humo tangu tarehe 14 mwezi uliopita licha ya kwamba shehena hizo zinahitajika ili kuokoa maisha ya watu.

WHO imetoa wito kwa pande zote husika kwenye mzozo nchini Yemen kuruhusu misafara hiyo na uwasilishaji kwa wahitaji wote bila kujali maeneo waliko.

Imekumbusha kuwa wakati wa mzozo, ni muhimu vituo vya afya vikasalia na utendaji kazi na kuwapatia watu huduma bila zahma yoyote.

(Sauti ya DKT. Shadoul)

“ Malori saba yaliyobeba vifaa yako karibu na mji wa Taiz na hayaruhusiwi kuingia ndani ya mji ili kusambaza vifaa hivyo kwa hospitali ndani ya mji. Bado Hatujaruhusiwa kuingia, na ni wiki ya nne sasa. “