Skip to main content

Afrika itumie vyanzo vya mapato ya ndani kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi: Ningu

Afrika itumie vyanzo vya mapato ya ndani kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi: Ningu

Licha ya kupitishwa kwa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP21,  bara la Afrika linahitaji kutumia vyanzo vya mapato ya ndani ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoeendelea kulikumba bara hilo  kwani kutegemea wahisani hakutakidhi haja amesema Mkurugenzi wa mazingira ofisi ya makamu wa Rais Tanzania Julius Ningu.

Katika mahojiano na idhaa hii kuhusu nini bara la Afrika lifanye, Bwana Ningu amesema mkataba wa COP21 ulizijumuisha nchi zinazoendelea lakini eneo la fidia ya fedha haikufikiwa kama ilivyotarajiwa kwa hiyo akashauri.

(SAUTI NINGU)

Kadhalika amesema ni muhimu Afrika ikachukua tahadhari ya kutosha kabla ya madhara zaidi ya tabianchi.

(SAUTI NINGU)