Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi kutoka kambi za Sudan kupewa makazi Ujerumani:IOM

Wakimbizi kutoka kambi za Sudan kupewa makazi Ujerumani:IOM

Ndege ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) imewasafirisha wakimbizi 179 wa Eritrea, Ethiopia na Syria ambao ni jumla ya familia 42, kutoka mji mkuu wa Sudan Khartoum kuelekea Kassel, Ujerumani kwenye makazi yao mapya.

Kabla ya kuondoka IOM Sudan imewafanyia tathimini ya afya na kuwapa chanjo wakimbizi hao ambao walikuwa wakiishi kwenye kambi mashariki mwa Sudan mpakani mwa Ethiopia na Eritrea. Wakimbizi hao ni pamoja na waEthiopia walioishi kambini hapo tangu miaka ya 1980 na familia ya waSyria waliowasili kambini 2014.