Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi na wahamiaji milioni 1 wakimbilia Ulaya 2015:UNHCR/IOM

Wakimbizi na wahamiaji milioni 1 wakimbilia Ulaya 2015:UNHCR/IOM

Mauaji , vita na umasikini vimewalizimisha watu milioni moja kukimbilia Ulaya mwaka 2015 kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji( IOM) .Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Kwa mujibu wa UNHCR kufikia tarehe 21 Desemba takribani watu 972,000 wamevuka bahari ya Mediterenia, huku IOM ikikadiria kwamba zaidi ya watu 34,000 wamevuka mpaka kutoka Uturuki na kuingia Bulgaria na Ugiriki kwa kutumia nchi kavu.

Mashirika hayo yanasema idadi ya watu waliotawanywa na vita na machafuko ni kubwa sana tangu ile iliyoshuhudiwa Ulaya Magharibi na Kati miaka 1990 wakati kulipozuka vita Yugoslavia ya zamani.

Mmoja kati ya wawili waliovuka mpaka , watu 500,000 miongoni mwao wamekimbia machafuko Syria, huku Afghanistan wakiwa asilimia 20 na Iraq asilimia 7. Kamishina Mkuu wa wakimbizi António Guterres amesema

(SAUTI YA GUTERRES)

“Wakati hisia dhidi ya wageni zikiongezeka katika baadhi ya maeneo ni vizuri kutambua mchango wa wakimbizi na wahamiaji katika jamii hizo ambazo wanaishi na kuheshimu misingi ya Ulaya ambayo ni kulinda maisha, kuzingatia haki za binadamu na kuchagiza kuvumiliana natamaduni mbalimbali”