Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunyongwa kwa mfanyakazi wa nyumbani Saudi Arabia kunasikitisha: Pillay

Kunyongwa kwa mfanyakazi wa nyumbani Saudi Arabia kunasikitisha: Pillay

Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea masikitiko yake kufuatia kitendo cha kunyongwa hadi kufa kwa mfanyakazi wa nyumbani Rizana Nafeek huko Saudi Arabia kwa kosa la kumuua mtoto wa mwajiri wake.

Msemaji wa Ofisi hiyo Rupert Colville amemkariri Pillay akisema kuwa adhabu hiyo ni kinyume na haki za binadamu kwa kuwa  Rizana raia wa Sri Lanka wakati anadaiwa kutenda kosa hilo hakuwa na umri wa mtu mzima na hata mazingira ya uendeshaji wa kesi yake yalikiuka haki za binadamu..

(SAUTI YA RUPERT)

Ofisi hiyo imeonyesha wasiwasi wake juu ya ongezeko la hukumu za kifo nchini Saudi Arabia na imeitaka nchi hiyo kuungana na nchi zingine duniani kuachana na adhabu ya kifo.