Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madawati ya jinsia yakomboa wanawake Tanzania

Madawati ya jinsia yakomboa wanawake Tanzania

Ukatili dhidi ya wanawake ni mlipuko unaokumba dunia! Hiyo ndiyo kauli inayopigiwa chepuo wakati huu ambapo kampeni ya siku 16 za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ikiwa imezinduliwa rasmi duniani kote hadi tarehe 10 mwezi ujao. Kampeni ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake inapigiwa chepuo kwa kuwa maisha ya wanawake na watoto wa kike yako hatarini maeneo mbali mbali duniani. Mathalani ndoa katika umri mdogo kwa watoto wa kike, ubakaji ndani ya ndoa, rushwa ya ngono, wanawake kunyimwa matumizi nyumbani na hata kutelekezwa.  Lakini sasa hatua zinaanza kuchukuliwa ikiwemo huko Tanzania ambako kumeanzishwa madawati ya jinsia ili kutoa fursa ya wanawake wanaodhulimiwa kuweza kusaka haki yao. Na hiyo ndiyo muktadha mzima wa Jarida letu maalum hii leo kama anavyokuletea Grace Kaneiya.