Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanaopata matibabu ya ukimwi kuendelea kuongezeka: UNAIDS

Idadi ya wanaopata matibabu ya ukimwi kuendelea kuongezeka: UNAIDS

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la ukimwi UNAIDS inasema mafanikio makubwa zaidi yamepatikana katika kupambana na ukimwi, yakionyesha matumaini ya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.

Takwimu zilizotolewa leo na UNAIDS zinaonyesha kwamba idadi ya vifo imepungua kwa asilimia 42 tangu mwaka 2004 na idadi ya watu wanaopata matibabu imefikia zaidi ya milioni 15, ikilinganishwa na milioni 22 mwaka 2005.

Taarifa ya UNAIDS imeeleza pia kwamba faida ya matibabu aina ya ARV ni kuwezesha watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kuishi maisha marefu na mazuri zaidi.

Ili kufikia lengo la kuongeza maradufu idadi ya watu wanaopata matibabu, UNAIDS imeeleza kwamba ni muhimu kufikia watu mapema iwezekanavyo wanapoambukizwa.