UNHCR yaonya juu ya janga jipya la kibinadamu Ulaya

UNHCR yaonya juu ya janga jipya la kibinadamu Ulaya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudumia wakimbizi UNHCR limeonya juu ya janga jipya  la kibinadamu kufuatia vikwazo katika mipaka dhidi ya wakimbizi na wahamiaji wanaosaka hifadhi katika ukanda wa kusini Mashariki mwa Ulaya

Taarifa ya UNHCR inasema kuwa kwa kushirikiana na wadau wengine kama vile shirika la kimataiafa la wahamiaji IOM, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, juma lililopita walionya juu ya hatari hiyo kutokana na mfululizo wa vikwazo vipya na visivyoratibiwa na kusema kuwa janga hilo linahitaji kutatuliwa kwa dharura.

Mashirika hayo yanasema kuwa vikwazo vipya vinadaiwa kuhusisha watu kutambuliwa kwa misingi ya mataifa yao ,mathalani katika mpaka kati ya Ugiriki na iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia ya Macedonia na katika mpaka kati ya Macedonia na Serbia raia kutoka Afghanistan, Syria na Iraq wanaruhusiwa kuvuka huku wengine wakizuiliwa.

Hali hii imesababisha takribani watu 1000 kusalia katika lango kuu la mpaka katia ya Macedonia na Ugiriki wasijue la kufanya.