Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugaidi wahatarisha shughuli za kibinadamu nchini Mali

Ugaidi wahatarisha shughuli za kibinadamu nchini Mali

Nchini Mali, zaidi ya wahudumu wa kibinadamu 30 wamefariki dunia tangu mwanzo wa mzozo kutokana na ghasia na ugaidi huku vitendo hivyo vikihatarisha usaidizi wa kibinadamu. John Kibego na ripoti kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Hii ni kwa mujibu wa Mbaranga Gasarabwe, Naibu Mwakilishi wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Mali na pia mratibu wa maswala ya kibinadamu nchini,  humo, alipozungumza na idhaa hii kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea wiki iliyopita kwenye hoteli mjini Bamako na kusababisha vifo 27.

Amesema hayo yametokea wakati mashirika ya kimataifa yalianza kuona nuru baada ya kusainiwa na kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya amani, mapigano baina ya pande za mzozo yakiwa yamesitishwa.

Hivyo amesema mashambulizi ya kigaidi yanazidi nchini humo, yakiathiri upelekaji misaada ya kibinadamu kwa wahitaji na hivyo amesama usalama kwa watoa misaada ya kibinadamu ni haki ya kimataifa ya kibinadamu.

(Sauti ya Bi Gasarabwe)

‘‘Tunafanya kazi katika eneo hilo, tunawafikia watu, na tunafanya vitu ambavyo wimbi la ugaidi haliwezi kutuzuia kwa sababu vinginevyo watafanikiwa na hatutaki hilo. Sisi ndiyo twapaswa kufanikiwa kwa maslahi ya binadamu .’’