Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi mbadala ya mkaa yanahitajika kunusuru mazingira Tanzania: Benki ya dunia

Matumizi mbadala ya mkaa yanahitajika kunusuru mazingira Tanzania: Benki ya dunia

Ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa unaotumika kwenye shughuli mbali mbali ikiwemo kupikia unatajwa kuwa fursa kubwa ya kipato nchini Tanzania ambapo wanajamii wengi hususani vijana huitegemea biashara hiyo kwa ajili ya ustawi wao.

Lakini biashara hii hutajwa kama moja ya vyanzo vya kuharibu mazingira kutokana na kukata miti,  ndiyo maana wadau wa mabadiliko ya tabianchi wanashauri matumizi bora ya mkaa au mbadala. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo kufahamu kile ambacho kinafanyika huko nchini Tanzania.