Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO na makampuni 11 yapigia chepuo haki za watu wenya ulemavu

ILO na makampuni 11 yapigia chepuo haki za watu wenya ulemavu

Shirika la kazi ulimwenguni ILO kwa kushirikiana na makampuni 11 ambayo yamekuwa wadau wa kwanza kusaini mkataba kuhusu ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika maeneo ya kazi wanapigia chepuo kundi hilo kote duniani .

Taarifa ya ILO inasema kuwa kazi hiyo ya kimataifa iliyoko  chini ya mkataba wa mtandao wa walemavu inahusu maeneo mengi ya ulinzi dhidi ya kundi hilo ikiwamo kuwalinda dhidi ya ubaguzi.

Shirika hilo la kazi ulimwenguni linasema kuwa kupinga ubaguzi kwa watu wenye ulemavu sehemu za kazi ni kwa kufanya mawasiliano na vifaa makazini yawe rafiki kwa wote wakiwamo kundi hilo.

Baadhi ya makampuni yaliyosaini mkataba huo ni pamoja na Michelin, Standard Bank Group na Accor Hotel.