Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulaya Mashariki waongeza nafasi za wahamiaji

Ulaya Mashariki waongeza nafasi za wahamiaji

Viongozi kutoka ukanda wa Ulaya Mashariki wamekubaliana kuandaa nafasi kwa ajili ya wahamiaji laki moja nchini Ugiriki na Ulaya Mashariki, kuongeza udhibiti wa mipaka na usajili.

Katika mkutano wa viongozi hao wamkubaliana katika mambo ya msingi 17 ikiwamo kuongea uwezo, kutoa malazi ya muda, chakula na huduma za afya, maji na huduma za kujisafi.

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR Antonio Guterres anasema nafasi kwa wahamiji 20,000 zaidi zinahitajika, huku akieleza wasiwasi kuhusu majira ya baridi kali.

(SAUTI GUTERRES)

"Tunawasiwasi mkubwa na dhoruba ya msimu wa baridi katika harakati ambayo mpaka sasa ni ya kusuasua kwa kupitia Balkans. Na muafaka ulioanzishwa ambao tunatumai utakuwa maamuzi, ya kuwa na sehemu 50,000 ambapo watu watawekwa, hatimaye sio tu yatasaidia kudhibiti harakati hizi, bali pia zitasaidia katika kutoa misaada ya kibinaadamu, ili kujikinga na janga ambalo linaweza kutokea pindi msimu wa baridi utakapofika."