Skip to main content

Zaidi ya watu milioni moja na nusu waangalia video ya Kulwa Tanzania

Zaidi ya watu milioni moja na nusu waangalia video ya Kulwa Tanzania

Nchini Tanzania, idadi ya mashambulizi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albinino imeongezeka mwaka huu, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu ikionya kwamba mwelekeo huu umesababishwa na kampeni ya uchaguzi inayofanyika mwaka huu na imani potofu za wagombea.

Katika jitihada zake za kuelimisha jamii kuhusu tatizo hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF liliandaa video iliokuwa ikionyesha maisha ya Kulwa, mischana mwenye ulemavu wa ngozi aliyepitia mateso kutokana na ulemavu wake.

Ilipofika kwenye mitandao ya kijamii, video hii ikatizamwa na watu wengi kutoka duniani kote wakitoa maoni yao ya kumfariji na kumpa moyo.

UNICEF na Shirika lisilo la kiserikali la Under the Same Sun yakaamua kumwonyesha Kulwa matokeo hayo. Ungana na Priscilla Lecomte kwenye Makala hii.