Amani na usalama wa kimataifa vyajadiliwa
Mjadala kuhusu amani na usalama wa kimataifa umefanyika hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati Umoja huo ukiadhimisha miaka 7o tangu kuanzishwa kwake.
Akichangia katika mjadala huo Rais wa Baraza Kuu Mogens Lykketoft amesema lazima chombo hicho kitatue changamoto za amani na usalama zinazotatiza dunia ikiwamo vikundi vya kigaidi na misimamo mikali, kwani bila kufanya hivyo dhana ya maendeleo haitatimia.
Kadhalika akazungumzia changamoto ya wahamiaji inayoikumba dunia kwa sasa akisema .
(SAUTI)
‘‘Jukumu letu katika amani na usalama, haki za binadmu na maendeleo lazima lieleze namna ya kushughulikia janga la wakimbizi . Ni muhimu tupitishe njia madhubuti katika yote tunayofanya .’’