Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kuongezeka maradufu: WHO

Idadi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kuongezeka maradufu: WHO

Leo ikiwa ni siku ya wazee duniani, imeelezwa kuwa maendeleo katika sekta ya tiba yamesababisha watu kuishi muda mrefu zaidi na kwamba idadi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 inatarajiwa kuongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2050, hali inayohitaji mabadiliko makubwa ya kijamii ikiwemo maendeleo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Hiyo ni kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya wazee ambapo shirika hilo linasema hii leo watu wengi, hata katika nchi maskini, wanaishi maisha marefu, lakini kuishi miaka mingi pekee haitoshi.

Dkt John Beard ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya na uzee akisema awali kasi ya ongezeko la wazee ilikuwa nchi zilizoendelea lakini sasa kasi ni kubwa nchi za kipato cha chini na kati na kwamba cha kusikitisha...

(SAUTI BEARD)

 “Mara nyingi tupozungumzia mpito kuelekea uzee, tunachukuliwa kwa fikra mbaya kwani wazee huonekana kama mzigo, watu dhaifu na gharama kubwa kuwatunza. Lakini ushahidi unaonyesha kuwa wazee wanachangia mara nyingi kwa njia zisizo rasmi au rasmi katika jamii zao na hata kwenye nguvu kazi .”