Skip to main content

UNICEF yakaribisha kupitishwa kwa SDGs

UNICEF yakaribisha kupitishwa kwa SDGs

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika linalohusika na maslahi ya watoto, UNICEF, Anthony Lake, amekaribisha uamuzi wa kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu, SGDs, akiutaja kama mwisho wa mchakato na mwanzo wa jitihada za kugeuza ahadi kuwa vitendo. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Katika taarifa, Bwana Lake amesema ingawa hatua za maendeleo zitapimwa kwa takwimu, kipimo halisi kitakuwa katika kila mtoto anayeinuliwa kutoka kwa umaskini, kila mama anayejifungua na kubaki hai, na kupitia kila msichana asiyepoteza utoto wake kwa ndoa za mapema.

Mkuu huyo wa UNICEF amesema, kwa kuwasaidia watoto maskini zaidi leo kwa kuwapa fursa bora maishani, minyororo ya umaskini uliokithiri ya siku zijazo inaweza kuvunjwa.