Skip to main content

Papa Francis awasili makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Papa Francis awasili makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis amewasili katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo kwa mujibu wa ratiba atakuwa na shughuli kadhaa ikiwemo kuzungumza na wafanyakazi wa umoja huo.

Mara alipowasili amelakiwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Papa Francis baada ya kukutana na kuzungumza na wafanyakazi anaweka shada la maua kukumbuka walinda amani waliopoteza maisha wakiwa wanahudumu kwa ajili ya amani duniani.

Hatimaye atahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kugusia masuala ya ajenda ya maendeleo endelevu inayopitishwa baadaye leo na nchi wanachama wa Umoja huo.