Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bi. Gamba kutoka Argentina kuongoza chombo cha uchunguzi kuhusu silaha

Bi. Gamba kutoka Argentina kuongoza chombo cha uchunguzi kuhusu silaha

Katibu mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Virginia Gamba kutoka Argentina kuongoza chombo cha uchunguzi cha pamoja cha umoja huo na shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali OPSCW.

Chombo hicho, JIM kiliundwa hivi karibuni kufuatia azimio namba 2235 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

Hadi anateuliwa, Bi. Gamba amekuwa ni Mkurugenzi na Naibu Mwakilishi mkuu kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kutokomeza matumizi ya silaha .

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa, Bi. Gamba atakuwa na manaibu wawili mmoja wa masuala ya siasa na mwingine masuala ya uchunguzi.

Katika taarif ahiyo, Katibu Mkuu Ban ametoa wito kwa pande husika nchini Syria kupatia chombo hicho ushirikiano wa kutosha akisema anatarajia ushirikiano thabiti kutoka Baraza la usalama na wanachama wote wa Umoja wa Mataifa katika kutekeleza azimio lililoanzisha chombo hicho.