Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo za nchi za kusini mwa dunia kuwaleta pamoja nyota wa muziki na filamu

Tuzo za nchi za kusini mwa dunia kuwaleta pamoja nyota wa muziki na filamu

Tuzo za mwaka 2015 za nchi za kusini mwa dunia zinatazamiwa kuwaleta pamoja wana Sanaa maarufu, wakiwemo wacheza filamu wa Hollywood, Robert De Niro na Michael Douglas, ambao watasaidia kupaazia sauti ufanisi wa ushirikiano wa nchi za kusini mwa dunia, kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, pamoja na kupitishwa kwa ajenda mpya ya mkakati wa maendeleo baada ya mwaka 2015.

Nyota wengine watakaoungana nao ni Mshindi wa tuzo ya Oscar, Forest Whitaker, akiwasilisha tuzo ya ufanisi wa kibinadamu kwa msamaria mwema William “Bill” Austin katika hafla itakayorushwa moja kwa moja kutoka hoteli ya Waldorf Astoria, mjini New York.

Tuzo hiyo ambayo imeingia mwaka wa tano, hutunukiwa nchi, watu binafsi na mashirika yanayowakilisha maendeleo endelevu yanayoleta mabadiliko kote duniani, hususan katika nyanja za kutokomeza umaskini, kuendeleza elimu na juhudi za kibinadamu.