Skip to main content

Ngoma ya Sega ni utambulisho wa watu wa Mauritius

Ngoma ya Sega ni utambulisho wa watu wa Mauritius

Utamaduni unatajwa kama kiungo muhimu katika jamii yeyote. Katika jamii ya watu wa Mautitius, ambao wanajivunia asili mbalimbali na lugha mbali mbali.Moja ya utamaduni ambao watu hawa wanajivunia ni ngoma ya kitamaduni ijulikanayo kama Sega Tipik.

Sega inajumuisha asili mbalimbali za watu wa Mauritius na inavunja migawanyo, inatoa fursa za upatanishi wa kitamaduni na unaimarisha uwiano wa urithi wa watu wa Mauritius.

Hii ni kulingana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Matiafa, UNESCO. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii ufahamu mengi kuhusu utamaduni huu.