Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi Haiti ni hatua muhimu kidemokrasia: MINUSTAH

Uchaguzi Haiti ni hatua muhimu kidemokrasia: MINUSTAH

Maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa na  Haiti wameungana na nchi wanachama wa UM katika kuunga mkono uchaguzi wa Rais , wabunge, viongozi wa mitaa na manispaa unaotarajiwa kufanyika mwezi August ulioelezwa ni hatua muhimu kwa nchi hiyo.

Taarifa ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH inasema uchaguzi huo unaoanza Agosti nane  na ambao huenda ukamalizika mwisho wa mwaka kutokana na kuwa na hatua kadhaa, ni muhimu kwa taifa.

Akongea kwenye  mkutano katika makao makuu ya MINUSTAH uliowahusiaha marafiki wa Haiti wakiongozwa na Uruguay, Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo aliye pia mwakilishi wa Katibu Mkuu Sandra Honoré, amesema ni fursa kuu kuthibitisha  ahadi ya pamoja katika uimarishwaji wa demokrasia na mshikamano  kwa matumaini ya watu wa Haiti.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Haiti Evans Paul ameihakikishia jumuiya ya kimataifa kuwa uchaguzi utafanyika katika mazingira salama na kuongeza kuwa kiasi cha dola milioni sita zimetengwa kwa ajili ya usalama wakati wa mchakato pamoja na dola miloini 10 za kuwezesha vyama shiriki .