Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Srebrenica yafanyika.

Kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Srebrenica yafanyika.

Maisha  maelfu ya watu yalikatishwa kinyume na sheria mjini Bosnia miaka 20 liyopita huko Srebrenica, nchini Bosnia na Herzegovina na mauaji hayo yatakumbukwa daima amesema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Elliason.

Alikuwa akizungumza jumamosi katika tukio la kumbukizi kijijini Potočari ambako watu 8000 wengi wao wakiwa wanaume na wavulana waislamu waliuwawa na waasi kutoka kundi la jeshi la Jamhuri ya Serbia mwaka 1995.

Bwana Eliasson amesema Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa ilishindwa  kulinda watu waSrebrenica na kuongeza kuwa zama za ukwepaji wa sheria zimekwisha kupitia mahakama ya kimataifa  uhalifu wa makosa ya jinai pamoja na kuteuliwa kwa mshauri maalum wa ulinzi dhidi ya mauaji ya kimbari mwaka 2004

Amesema anatamani kuwa mauaji ya kimbari yaliyotokea yangefanya dunia kutambua kuwa laana ya ya chuki na madhara ya migawanyiko.

 

Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa bado machafuko yanaendelea vibaya nchini Syria, Iraq na Sudan Kusini na Yemen na sehemu nyinginezo.

Bwana Eliasson ameongeza kuwa maadhimisho ya mauajia ya kimbari ya Srebrenica yatumike kutoa ahadi kuwa chuki haiwezi kushindwa kwa chuki na kuwa kumbukumbu za waliowawa lazima ziheshimiwe kwa kusaka kuifanya dunia kuwa bora zaidi.