Skip to main content

Ban ahudhuria kumbukizi ya vita kuu ya pili ya dunia, akutana na Putin

Ban ahudhuria kumbukizi ya vita kuu ya pili ya dunia, akutana na Putin

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon jumamosi hii ameshuhudia gwaride la ushindi katika eneo liitwalo Red Square mjini Moscow nchini  Urusi, ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 70 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia ikiwa ni matokeo ya kujisalimisha kwa utawal wa kinazi nchini Ujerumani.

Katika ziara yake hiyo nchini Urusi Bwana Ban pia amekutana na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin.

Pia amekutana na kufanya mazungumzo Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades.

Katibu Mkuu ameanza ziara yake nchini Poland alhamisi ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kumaliziaka kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Kumbukizi ya miaka 70 tangu kumalizika kwa vita hiyo ni muhimu kwa Umoja wa Mataifa kwani vita hiyo iliweka msigi wa  kuanzishwa kwake baada ya vifo vya mamilioni ya watu.

Katibu Mkuu Ban ameelekea Ukraine ijumaa kwa ajili ya kumbukizi ya wanajeshi mashujaa wa nchi hiyo waliopigana dhidi ya utawala wa kinazi kwa lengo la kuishi kwa amani na utulivu.