Wakimbizi wa ndani waongezeka maradufu Libya: UNHCR

Wakimbizi wa ndani waongezeka maradufu Libya: UNHCR

Idadi ya wakimbiz iwa ndani nchini Libya imeongezeka mara mbili zaidi ikilinganishwa na idaid ya awali mwaka jana mwezi Septemba kutokana na kuongezeka kwa machafuko sehemu mbalimbali mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbuizi UNHCR  mwaka jana idiadi hiyo ilikuwa 230,000 ambapo mwaka huu idadi hiyo imefikia 434,000. Wakimbizi wa ndani wanjumuisha familia 83, 697 kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na UNHCR nchi nzima.

UNHCR na washirika wake kutoka katiak mamalaka za ndani ya Libya ikiwamo asasi za kiraia , imekuwa ikisaidia wakimbizi wa ndani ambapo chakula na misaada isiyo ya chakula imekuwa ikitolewa.

Shirika hilo la wakimbizi linasema kuwa idaidi hiyo yaweza kuwa kubwa zaidi kwani hawajafinikiwa kuyafikia maeneo yote kutokana na machafuko yanayoendelea .