Kuna fursa nyingi za kimaendeleo ukanda wa maziwa makuu: Djinnit
Ukanda wa maziwa makuu barani Afrika sio tu kuwa una idadi ya watu wanaoweza kufanya kazi bali pia una soko na fursa za uwekezaji katika sekta muhimu ikiwamo kilimo na nishati amesema Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda huo Said Djinnit.
Akiongea katika mkutano kuhusu biashara kwa amani mjini New York uliongazia ujenzi wa amani na kutambua maendeleo endelevu Bwana Djinnit ametaja maeneo mengine ambayo ukanda wa maziwa makuu unaweza kuwekeza ni madini, utalii, mawasiliano na teknolijia nakuongeza kuwa ukanda huo unakabiliana na ongezeko kubwa la watu.
Amesema ofisi yake inafanyakazi kwa kushirikiana na kongamano la kimataifa la ukanda wa maziwa makuu (ICGLR) na wadau wengine wakiwamo muungano wa Afrika AU ili kuandaa mkutano kuhusu uwekezaji wa sekta binafsi kwa ajili ya nachi za maziwa makuu mjini Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo maalum wa Umoaj wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu, mkutano huo uanatarajiwa kuwa hatua muhumu katika mashirikianao baina ya kampuni, wawekezaji na wadau wengine katika ukanda.