Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon akaribisha kusainiwa kwa makubaliano ya amani Mali

Ban Ki-moon akaribisha kusainiwa kwa makubaliano ya amani Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kusainiwa leo mjini Bamako kwa makubaliano ya amani na maridhiano nchini Mali na jumuiya ya vikundi vilivyojihami.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Bwana Ban amenukuliwa akipongeza pande za mzozo na timu ya uhamasishaji iliyoongozwa na Algeria kwa jitihada zao katika kufanikisha utaratibu huo.

Amesema makubaliano hayo ni hatua ya kwanza katika utaratibu wa amani, akisisitiza kwamba ni wajibu wa Mali na raia wake kukuza amani, akizisihi pande zote kuendelea kushirikiana kwa nia nzuri na kutekeleza vilivyoamuliwa.

Katibu Mkuu amekariri utayari wa Umoja wa Mataifa wa kuzisaidia pande zote katika kutekeleza makubaliano hayo, ili kuleta amani ya kudumu nchini humo.