Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asisitiza haki za binadamu kwa amani na maendeleo Uzbekistan

Ban asisitiza haki za binadamu kwa amani na maendeleo Uzbekistan

Akiwa ziarani nchini Uzbekistan Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema hakuna amani na maendeleo ikiwa hakuna haki za binadamu. Tarifa zaidi na Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Akiongea na vyombo vya habari nchini humo Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya kamishna mkuu wa haki za binadamu iko tayari kusaidia Uzebikistan katika kukuza na kulinda haki za msingi na kutoa fursa kwa uma kushiriki ikiwamo kupitia vyombo huru vya habari, taasisi za kidemokraisa, upatikanaji wa haki pamoja na uhuru wa asasi za kiraia.

Ban amesema Umoja wa Mataifa uko bega kwa bega na nchi hiyo katika kuunga mkono jitihada za amani na usalama katika ukanda huo kupitia kituo chake cha diplomasia ya ulinzi kwa ajili ya Asia ya Kati.

Katika muktadha huo Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa uko tayari  pia katika usaidizi nchini humo ili kuhakikisha watetezi wa haki za binadamu wanatekeleza majukumu yao aliyoyaita muhimu huku pia akisema haki za binadamu ndiyo ishara ya jamii imara na inayoelekea katika mafanikio.

Bwana Ban amesifu uanzishwaji wa sheria njema na akasisitiza kuwa sheria hizo zisisalie vitabuni pekee bali ziwe halisi katika maisha ya kila siku ya wanajamii.

Amepongeza taifa hilo kwa kukomesha ajira za watoto hususan katika sekta ya mkonge na kutoa wito wa kushughulikia hamasisho la walimu na madaktari  na wengineo katika uvunaji wa mkonge na ulinzi wa ukatili dhidi ya wafungwa.