Wajibu wa kutokomeza njaa usipuuzwe: Pope Francis

11 Juni 2015

Jamii ya kimataifa inapaswa kuitikia wito wa kimaadili wa kuhakikisha kila mtu anapata chakula kwa kuwa hiyo ni haki ya msingi ya kila mtu.

Ni kauli ya kiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Pope Francis aliyotoa kwenye kikao maalum cha mkutano wa mkuu wa 39 wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO huko Vatican, Italia.

Amesema iwapo nchi wanachama zitasaidiana, makubaliano ya kuchukua hatua ya FAO yatatekelezwa mapema na zaidi ya hapo jukumu la awali la FAO la kila mtu apate mlo lililopo kwenye nembo ya shirika hilo, litafikiwa.

Hata hivyo Pope Francis amesisitiza umuhimu wa kupunguza chakula kinachotupwa, kuelimisha umma kuhusu lishe na kujenga utambuzi wa dunia nzima juu ya umuhimu wa kila mtu kuwa na uhakika wa chakula.

Takwimu za FAO zinaonyesha kuwa theluthi moja ya chakula chote kinachozaliwa duniani kinatupwa au kinapotea wakati au baada ya mavuno.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter