Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wasaliwa na changamoto zaidi duniani: Ripoti

Watoto wasaliwa na changamoto zaidi duniani: Ripoti

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa leo zimepokea ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu watoto katika mizozo inayoonyesha mwelekeo wa athari za mizozo kwa watoto kwa mwaka 2014.

Ripoti hiyo imesema changamoto za ulinzi wa mtoto ni dhahiri kwa mamilioni ya watoto wanaokulia kwenye maeneo kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati, Iraq, Israel, Nigeria Sudan Kusini, Syria na Palestina.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric anaweka bayana alipozungumza na waandishi wa habari maeneo ambako bado hali inazidi kuwa mbaya kwa watoto.

(Sauti ya Dujarric)

Bado kuna matukio ya kuendelea kwa ukiukwaji wa haki dhidi ya watoto kwenye mizozo iliyokithiri kama vile Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Somalia. Na hivi karibuni zaidi hali ya usalama Yemen imezidi kuzorota kufuatia ripoti za Aprili mwaka huu ambapo idadi ya watoto wengi ni wahanga.”