Ukiukaji wa haki za binadamu Eritrea ni mkubwa: ripoti

8 Juni 2015

Serikali ya Eritrea inatekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, huku raia wakiteswa, kufungwa, kuawa bila sababu, au kutumikishwa jeshini bila ukomo, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo. Baadhi ya ukiukaji huo unaweza kutambuliwa kama uhalifu wa kibinadamu.Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Ripoti hiyo inasema kuwa mfumo wa usalama nchini Eritrea unachunguza raia wa Eritrea kwenye kila ngazi ya jamii na kusababisha watu kuishi kwa wog na imetolewa  wakati huu ambapo jamii ya kimataifa inakumbwa na idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi wakijaribu kufika Ulaya au Mashariki ya Kati, wengi wao wakiwa ni Waeritrea.

Sheila B. Keetharuth ni Mtalaam Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Eritrea.

“Wanakimbia nchi inayotawalwa kwa woga, si sheria. Ripoti yetu inasema kwamba vijana wa Eritrea wanaishi bila matumaini kabisa, wajihisi hawana njia ya kuleta mabadiliko na Mamia ya maelfu wanakimbia nchi wakiwa hatarini  kukamatwa na kuteswa na mamlaka za Eritrea au kuuawa na wasafirishaji haramu. Wanastahili ulinzi wa kimataifa” 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter