Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahaha kusajili Warohingya walioko Bangladesh

UNHCR yahaha kusajili Warohingya walioko Bangladesh

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaendelea na harakati za kupata fursa ya kuweza kusajili watu wa jamii ya Rohingya kutoka Mynmar ambao wako nchini Bangladesh.

Umoja wa Mataifa kupitia msemaji wake umeeleza kuwa warohingya hao wapatao Laki Mbili hawako kihalali nchini humo licha ya UNHCR kuwatambua kuwa ni wakimbizi tangu Januari mwaka 2010.

Hadi sasa UNHCR haijaweza kuwafikia na kuwasajili na kuwapatia nyaraka zozote za kuwasaidia.

Kwa mujibu wa UNHCR wakimbizi hao wanaishi na wenyeji wakati huu ambapo Bangladesh inaelezwa haiko katika mazingira mazuri kukabiliana na uwepo wa wakimbizi hao kutokana na umaskini, kiwango kikubwa cha ongezeko la idadi ya watu na majanga ya asili yanayokumba nchi hiyo mara kwa mara.