Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya mazingira duniani darubini zikielekea Uganda

Siku ya mazingira duniani darubini zikielekea Uganda

Mazingira, mazingira,mazingira!

Hii ni sauti inayopazwa na  wadau wa mazingira kote duniani katika kuadhimisha siku hii adhimu ambayo mwaka huu imebeba ujumbe wa uboreshwaji wa mienendo ya matumizi ya raslimali.

Mwaka huu, kauli mbiu ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo inaadhimishwa Juni tano , ni 'Ndoto bilioni saba. Sayari Moja. Tumia kwa kujali.'  Wito unaohimiza raia kote ulimwenguni  kutafakari kuhusu mienendo yao ya maisha na kupunguza athari za vitendo vya wanadamu kwa rasilmali za asili kwa kufanya maaumuzi ya matumizi yenye busara. Katika mukatadha huo Katibu Mkuu wa Umoja waMataifa Ban ki- Moon ametaka matumizi ya bidhaa ambazo hazitumii kiwango kikubwa cha nishati, maji na rasilimali. Katika ujumbe wake wa siku hii ya mazingira duniani Bwana Ban ameangazia umuhimu wa maendeleo enedlevu unaiozingatia uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya mustakabali mwema wa sayari dunia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP ambalo ndilo limeshika uskuni wa hamasa ya kutunza mazingira linasema kupitia jopo lake la kimataifa kuhusu rasilmali kuwa iwapo mienendo isiyo endelevu ya matumizi na uzalishaji itaendelea, basi ifikapo mwaka 2050, rasilmali za asili zitakazotumiwa kudumisha mienendo hiyo zitakuwa ni sawa na zile za sayari tatu.

Barani Afrika juhudi za kutunza mazingira zikoje? Kutoka Uganda tuungane na John Kibego ambaye pamoja na mambo mengine anaeleza mkakati wa kisera na utekelezaji wake katika kuhifadhi  mazingira katika nchi hiyo ya Mashariki mwa  Afrika.