Skip to main content

Mwanamuziki Fally na harakati za kubadili maisha kuptitia kilimo

Mwanamuziki Fally na harakati za kubadili maisha kuptitia kilimo

Kila uchao vipaji vya muziki vinaibuka barani Afrika! Vijana wake kwa waume wanajikita katika sanaa hii ya muziki kuburudisha, kuelimisha na kuhabarisha. Hata hivyo Benki ya Dunia kupitia mradi wake wa Muziki kwa Maendeleo  #Music4Dev inashirikiana na wanamuziki kupambanua kile ambacho wanafanya ili kudhihirisha kuwa siyo tu mashujaa jukwaani bali pia ni mashujaa katika kubadili maisha ya kule wanakotoka. Miongoni mwa wanamuziki hao ni Fally Ipupa kutoka DR Congo ambaye katika makala hii inayosimuliwa na Assumpta Massoi inaeleza bayana kile anachofanya na ndoto yake kwa bara la Afrika.