Skip to main content

Ban ahuzunishwa na ajali ya meli China

Ban ahuzunishwa na ajali ya meli China

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameeleza kuhuzunishwa na vifo vya watu wengi kufuatia ajali ya meli ya abiria kwenye mto wa Yangtze, Uchina.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wake, Katibu Mkuu ametuma risala za rambirambi kwa familia za wahanga, na pia kwa serikali na watu wa Uchina.

Taarifa hiyo pia imemnukuu Ban akielezea matumaini yake kuwa manusura zaidi watapatikana.