Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko mapya Sudan Kusini yalaaniwa na UM

Machafuko mapya Sudan Kusini yalaaniwa na UM

Viongozi mbalimbali wamelaani hatua ya kuibuka upya kwa mapigano dhidi ya raia nchini Sudan Kusini kati ya vikosi vya serikali SPLA na vile vya upinzani SPLA-IO katika majimbo ya Unity na Upper Nile ambapo waathiriwa wakubwa ni wanawake na watoto.

Katika tamko la pamoja la viongozi hao akiwamo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa kuhusu ukatili wa kijinsia vitani Zainab Hawa Bangura, mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu watoto kuhusihwa vitani Leila Zerrougui, Mkurugenzi mkuu wa wa Shirika la wanawake katiaka Umoja wa Mataifa Phumzile Mlambo-Ngcuka wamesema kuwa taarifa zinasema tangu katikati ya mwezi April ukatili mkubwa na uvunjaji wa haki za binadamu za kimataifa unaendelea nchini humo .

Viongiozi hao wakiwamo pia mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia mauji ya kimbari Adama Dieng na mshauri wa UM katika jukumu la ulinzi Jennifer Welsh wamepinga kuendelea kwa machafuko, mauaji, utekwaji nyara wa wanawake na watoto, ubakaji na aina nyingine za ukatili wa kijinsia pamoja na matumizi ya watoto vitani, uporaji na uharibifu wa mali.