Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi walioko Burundi warejea makwao kuhofia usalama: UNHCR

Wakimbizi walioko Burundi warejea makwao kuhofia usalama: UNHCR

Sintofahamu ya machafuko inayoendelea nchini Burundi imesababisha baadhi ya wakimbizi kutoka nchi jirani mathalani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kurejea makwao huku wengine wakiomba kuhamishiwa katika kambi zilizoko nje ya mji mkuu Bujumbura.

Katika mahojiano na idhaa hii kutoka Burundi mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi  UNHCR nchini  humo Abel Mbilinyi amesema kuzorota kwa usalama nchini humo kumeathiri ustawi wa wakimbizi licha ya kwamba idadi ya wanaokimbilia nchijirani imepungua.

(SAUTI MBILINYI)

Amesema UNHCR inahakikisha wakimbizi wanakuwa salama hususani wakati huu ambapo mchakato wa uchaguzi unatarajiwa kuanza mwezi June katiak ngazi mbalimbali ikiwamo ya Rais .