Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maandalizi ya kuwaenzi mashujaa walinda amani yakamilika: DPKO

Maandalizi ya kuwaenzi mashujaa walinda amani yakamilika: DPKO

Matukio kadhaa yanatarajiwa kujiri hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa ambayo hufanyika May 29 kila mwaka. Kati ya matukio hayo ni utolewaji wa medali kwa mabalozi wa nchi wanachama ambazo walinda askari wake wako katika operesheni za ulinzi wa amani.Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii, Mnadhimu Mkuu wa Ofisi ya Kijeshi ya Idara ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed anaanza kuelezea maana halisi ya siku ya kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

(SAUTI MAHOJIANO)