Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yatoa huduma za afya kwa watoto wakimbizi kutoka Burundi walioko Tanzania

UNICEF yatoa huduma za afya kwa watoto wakimbizi kutoka Burundi walioko Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema asilimia 85 ya wakimbizi wanaoingia Tanzania ni wanawake na watoto na tayari wamebaini 1,000 ambao wamekimbia bila kusindikizwa na mtu wewote hivyo limnaanisha changamoto wanazikumbana na watoto hao ikiwamo utapiamlo.

Katika mahojiano na idhaa hii mtaalamu wa lishe wa UNICEF kutoka Tanzania Elisabeth Macha amesema licha ya kwamba idadi ya waliogundulika kuwa na utapiamlo si kubwa kati ya 9000 waliopimwa hadi sasa lakini wanachofanya ni..

(SAUTI ELISABETH)

Amesema vipimo na huduma nyinginezo kwa sasa zinafanyika katika kambi ya Nyarugusu nakuongeza kuwa usajili wa wakimbizi utakapokamilika kwa wakimbizi wengine huduma hizo zitafanyika pia.