Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji wa fedha wahitajika zaidi kuhakikisha upatikanaji nishati ifikapo 2030

Uwekezaji wa fedha wahitajika zaidi kuhakikisha upatikanaji nishati ifikapo 2030

Mkutano wa kila mwaka kuhusu nishati endelevu unamalizika leo mjini New York huku wadau kutoka nchi na mashirika mbalimbali wakikubaliana kusongesha mbele juhudi za upatikanaji zaidi wa nishati ambayo kwa sasa imewafikia watu zaidi ya milioni 90. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(TAARIFA YA MSAMI)

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, mabilioni ya dola yanahitajika katika mkakati wa nishati endelevu ili kupunguza umaskini unaosababishwa na ukosefu wa nishati duniani na kuongeza kuwa uwekezaji zaidi unahitajika katika kukabiliana na changamoto pacha ambazo ni umaskini unaotokana na ukosefu wa nishati na mabadiliko ya tabianchi.

Kadhalika makubaliano yaliyofikiwa yanataka serikali, mashirika ya kimataifa ,taasisi za kifedha na biashara pamoja na asasi za kiraia zinazojihusisha na nishati zinapaswa kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 malengo ya upatikanaji wa nishati endelevu yanatimia.

Katika mahojiano na idhaa hii muda mfupi baada ya uzinduzi wa mpango wa nishati kwa wote mkurugenzi mtendaji wa wakala wa uhusishaji wa nishati Irena Adnan Amin amesema ana matumaini kuwa bara la Afrika litapata nuru ya nishati lakini akisisitiza nini kifanyike.

(SAUTI AMINI)